Tuesday, 9 September 2014

MIKAKATI YA NCHI ZA MAGHARIBI KUWAGAWA WAISLAMU

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani B. Hilary Clinton amefichua mafanikio makubwa waliyoyapata Marekani na Ulaya tangu kulipoanzishwa kundi la Answari Suna (Uwahabi) na kwamba juhudi kubwa za Uingereza katika kuasisi kundi hilo limefanikisha kuzaa matunda ya kuzaliwa tena kundi la kigaidi linalojiita eti Dola la Kiislamu nchini lraq na Sham (Daesh au ISIS).
Katika kitabu hicho ambacho amekipa jina la 'Maamuzi Magumu' Clinton amesema kuwa, katika hali ambayo Waingereza waliasisi Uwahabi kwa kumpatia fedha nyingi mwasisi wa kundi hilo 'Muhammad lbn Abdul-Wahhabi, msaada ambao uliambatana na kumtaka aanzishe wimbi la kuharibu athari zote za Kiislamu kwa kuziita bidaa, yeye (Clinton) alikuwa na mchango wa kuanzishwa kundi la ISIS, ikiwemo kuwapatia silaha na fedha viongozi wake. Ameongeza kuwa, kwa kuasisiwa Uwahabi, wamefanikiwa kuwagawa Waislamu na kuwafanya Waislamu wa madhehebu ya Kisuni wawaone Mashia wanaoibukia kuwa na nguvu duniani na kuwa tishio kwa nchi za Marekani na waitifaki wake, kuwa makafiri, huku ISIS nayo ikiyasogeza malengo ya Marekani kwenye mafanikio ya kuzigawa nchi za Kiarabu, njama ambazo kwa miaka mingi zilishindikana kufikiwa.
Katika kitabu hicho ameweka wazi namna kundi la ISIS na makundi mengine kadhaa yaliyipigana nchini Syria na lraq, yanavyopewa msaada wa silaha kutoka Marekani na madola ya Ulaya na kwamba nara ya 'Jihadi' inayotumiwa na makundi hayo duniani ni daraja muhimu sana kuelekea mafanikio hayo.
Hii ni katika hali ambayo wasomi wengi wa Kiislamu na wasio Waislamu wamekuwa wakionya kila mara juu ya hatari inayoukabili ulimwengu wa Kiislamu na dunia kwa ujumla kutokana na kundi hilo la Kiwahabi ambalo sasa limekuwa likiwaita Waislamu wengine kuwa ni makafiri na kuhalalisha damu na mali zao, na kwamba kundi la ISIS na mengineyo kamavile, Boko Haram, ash-Shabab, Jab'hatu Nusra, al-Qaida, Taleban, Answaru Sharia, Mujao nk, ni vibaraka wa madola ya kibeberu.
Watu wamekuwa wakihoji mahala makundi yote hayo kote duniani yanakopata silaha, na fedha za kuendeshea harakati zake ambapo aghlabu huwezi kuyakuta makundi hayo yakifanya biashara yoyote ili kujiingizia kipato. Lakini cha ajabu siku hadi siku na wiki hadi wiki, mwezi hadi mwezi mwaka na miaka, makundi hayo yanazidi kupata nguvu na ustawi zaidi.
Aidha jambo jengine la kushangaza ni kuwa, daima na licha ya viongozi wa makundi hayo kuitwa majina mabaya na kutangazwa kutafutwa kwa udi na uvumba, maneno ambayo ni njama za kuwahadaa walimwengu, huwezi kusikia hata siku moja mmoja wa viongozi wa makundi hayo akitiwa mbaroni na nchi hizo zinazojinadi kuwa zinapinga ugaidi.
Watu wanauliza kuwa, inakuwaje viongozi wa makundi hayo hawawezekaniki kutiwa mbaroni hata kidogo? Kuna siri gani?
Kadhia ya Osama ilikuwa hivyo hivyo, Mulla Omar hadi leo hatujui yuko wapi lakini tunaambiwa yuko hai, Naibu wa Osama, Abubakar al-Baghdad na wengine wengi. Tunadanganywa tu. Je nikweli Marekani na nchi za Ulaya zimeshindwa kuwatia mbaroni watu hao? Au ndio kwanza nchi hizo ndizo zinazowapa hifadhi wahalifu hao ambao wapo kwa ajili ya kuuangamiza Uislamu?
Tafakari sana, kwani huu ni wakati wako wa kuchukua uamzi.

No comments:

Post a Comment