Friday 12 September 2014

VITABU VYA HADITH VINAVYOCHAPISHWA SIKU HIZI VINACHAKACHULIWA

VITABU VYA HADITH VINAVYOCHAPISHWA SIKU HIZI VINACHAKACHULIWA KUONDOA MADAI YA MASHIA KAMA WANAVYOFANYA WAKRISTO KUONDOA ATHARI ZA UISLAMU KWENYE BIBLIA.
mengi ya matoleo mapya ya vitabu hivyo yamefanyiwa mabadiliko na baadhi ya sehemu kuondolewa, hususan zile zinazounga mkono madai ya Shia. Ufuatao hapa chini ni mfano mdogo tu wa yanayofanywa katika
vitabu hivyo:
Katika ukurasa wa 301 wa juzuu ya 3 ya Tafsir al-Kashshaaf iliyokusanywa chini ya maelekezo ya Sheikh Mustafa al-Halabi (toleo la pili, 1319 A.H. liliochapishwa na Main Government Printing House ya Amiriah Bulaq ya Misir), kuna beti zinazojitokeza ambazo kwazo Jarullah Zamakhshari, mfasiri wa al-Kashshaaf, alitangaza wazi imani yake katika
uhalali wa Ushia. Lakini katika chapisho la 1373 A.H. lililochapishwa na Printing House Istiqamah bi’l-Qahara, shairi lililotajwa halionekani tena.
Marehemu Allamah Sayyid Akhtar Rizvi katika kitabu chake Uimamu uk. 37, anaandika kushangazwa kwake kutokana na maneno yaliyoondolewa katika kitabu cha at-Tarikh cha at-Tabari, chapa ya Leiden (ya mwaka 1879 Masihia) ambayo imeyanakili maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliyoyatumia wakati wa karamu maarufu ya ndugu wa karibu aliyoitayarisha mwenyewe.
Maneno ya mwisho aliyoyasema Mtukufu Mtume (s.a.w.) katika karamu hiyo yalikuwa haya: “Enyi watu wangu! Huyu Ali ni ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu miongoni mwenu; msikilizeni na mtiini.” Lakini katika chapa ya Misri (ya mwaka 1963 Masihia) - chapa ambayo inayodaiwa kuwa imechekiwa na ile ya Leiden - maneno haya muhimu:
“wasii wangu na khalifa wangu” yamebadilishwa na kuwa “kadha wa kadha” na kusomeka hivi: “Huyu Ali ni ndugu yangu na kadha wa kadha.” Huu ni msiba mkubwa.

No comments:

Post a Comment