Friday 12 September 2014

KWA NINI WAISLAMU WANARUDI KWENYE ENZI YA UJINGA YAANI KABLA YA UISLAM.

KWA NINI WAISLAMU WANARUDI KWENYE ENZI YA UJINGA YAANI KABLA YA UISLAM.
Anasema G.E. Grunebaum:
"Katika karne ya kabla ya kuja Uislamu makabila yalitawanya nguvu zao zote katika vita vya kuviziana, wote dhidi ya wote."
(Classical Islam - A History 600-1258-1970)
Yale makabila ya wahamaji yalizunguka kwenye peninsula yote na kupora misafara na makazi madogomadogo. Misafara mingi na vijiji vilinunua kinga ya mashambulizi Haya kwa kulipa kiwango maalum cha fedha kwa watekanyara wa wahamaji.
Ni muhimu kuzingatia ule ukweli katika usiku wa kuzaliwa Uislamu hakukuwa na serikali katika ngazi yoyote katika Arabia, na ukweli huu unawezakuwa umeathiri kuinukia kwa Uislamu wenyewe. Ukosekanaji mzima wa serikali, hata katika hali ya kuanzishwa tu, ni kitu kisichokuwa cha kawaida kabisa kwamba kimeonwa na kutolewa maoni na mus-tashirik wengi, miongoni mwao ni:
D.S. Margoliouth:
"Arabia ingebakia ya kipagani angekuwapo mtu katika Makka ambaye angeweza kutoa pigo; ambaye angeweza kutenda. Lakini wengi wao, kama walivyokuwa wabaya wa Mohammed, hapakuwa na mmoja wao aliyekuwa na ujasiri wa namna hii; na (kama ilivyoonekana) hapakuwepo na mahakimu kwa ujumla ambao kwao angeweza kushitakiwa."
(Mohammed and the Rise of Islam, 1971).
Naye Maxime Rodinson asema:
"Mauaji ya halaiki yalibeba adhabu kubwa kwa mujibu wa sheria zisizoandikwa za jangwani. Katika utendaji waarabu huru walikuwa hawakufungwa na kanuni ya sheria zake kwa msaada wa jeshi la polisi. Ulinzi pekee wa maisha ya mtu ni ile hakika iliyowekwa na mila na desturi, ambayo ingenunuliwa kwa gharama kubwa. damu kwa damu na uhai kwa uhai. "
(Mohammed, 1971) Asema Herbert J. Muller:
"Katika Arabia ya Mohammed hakukuwa na dola kulikuwa tu na makabila huru yaliyotangaa na miji. Huyu Mtume (s.a.w.) aliunda dola yake mwenyewe, na aliipa sheria tukufu iliyoandikwa na Allah (s.w.t.)"
(The Loom of History, 1958)
Watu wa Arabia walitokana na makundi mawili, wenye maskani na wahamiaji. Hijazi na Arabia ya Kusini ilitapakaa miji mingi midogo na mikubwa michache. Nchi yote iliyobakia illikuwa na watu waliotapakaa wakitokana na Mabedui. Walikuwa nyuma katika dhana ya uraia na siasa lakini pia walikuwa ni chanzo cha wasiwasi na hofu kwa wale wenye maskani. Waliishi kama maharamia wa jangwani, na walikuwa na sifa mbaya kwa ubinafsi wao usiozuilika na vurugu zao za upambanuzi wa kikabila.
Yale makabila maarufu zaidi yalitumia kiwango maalum cha mamlaka katika maeneo yao husika. Katika Makka kabila lenye nguvu lilikuwa la Quraishi, katika Yathrib, makabila yenye nguvu yalikuwa ni yale makabila ya Kiarabu ya Aus na Khazraji, na makabila ya kiyahudi ya Nadhir, Qaynuqa'a na Quraydha. Maquraishi wa Makka walijiona wenyewe ni bora kuliko Mabedui lakini hawa Mabedui walikuwa na dharau tu juu ya hawa watu wa mjini ambao kwao wao walikuwa ni "Taifa la wauza maduka tu".
Waarabu wote walikuwa na sifa mbaya kwa namna fulani ya tabia kama vile majivuno, kiburi na majisifu, ulipizaji kisasi na kupenda kwingi uporaji. Kiburi chao kilihusika kwa namna fulani na kushindwa kwao kuanzisha dola yao wenyewe. Walikosa nidhamu ya kisiasa, na mpaka kuja kwa Uislamu, hawakutambua mamlaka yoyote kama ni yenye umuhimu mkubwa katika Arabia.
Walitambua mamlaka ya mtu aliyewaongoza kwenye uvamizi lakini angeweza kulazimisha utii wao ikiwa tu walikuwa na uhakika wa kupata mgao mzuri wa ngawira, na mamlaka yake yaliisha mara tu shughuli hiyo ilipokwisha.
CHA KUSHANGAZA KARNE 14 BAADA YA KUWA WAISLAMU, BAADHI YA WAISLAMU WANADESTURI ZILEZILE ZA UJIMA. HAWATAKI KUITII SERIKALI YOYOTE, VISASI NI IBADA KWAO, HAWANA UTII SI KWA VIONGOZI WA SERIKALI BALI HATA MASHEIKH WAO WENYEWE. SI AJABU KUSIKIA MWANAFUNZI AKIMKUFURISHA MWALIMU WAKE. HUU NI MSIBA MKUBWA KATIKA UMMA HUU WA KIISLAMU

No comments:

Post a Comment