Friday, 12 September 2014

HASHIM - KABLA YA KUZALIWA UISLAMU sehemu ya pili

Uongozi wa uongofu na wema na ukarimu zilikuwa ni mbili tu kati ya sifa nyingi ambazo Muhammad, nabii wa baadaye, "alizorithi" toka kwa mababu zake. Hashim alioa mwanamke wa Yathrib na kutokana naye alipata mtoto wa kiume - Abdul-Muttalib. Kwa wakati upasao, Abdul Muttalib alikuwa amrithi baba yake kama mkuu wa ukoo wa Hashim.
Edward Gibbon:
"Huyu babu yake Muhammad (Abdul Muttalib), na nasaba yake ya jadi, wanaonekana katika kumbukumbu za kigeni na za ndani kama mabwana (wafalme) wa nchi yao; lakini walitawala, kama Percales huko Athens, au Medics huko Florence, kwa maoni ya hekima zao na msimamo; athari zao ziligawanyika pamoja na urithi wao. Kabila la Kuraish walijipatia usimamizi wa Al-Kaaba; ile ofisi ya kikasisi iliyoendelezwa kupitia mishuko minne ya nasaba hadi kwa babu yake Muhammad; na ukoo wa Hashim, kutoka pale alipochipukia, lilikuwa ndio liliheshimiwa sana na tukufu kwenye macho ya nchi yao.
Mshuko wa Muhammad kutoka kwa Ismail ulikuwa ni hadhi ya taifa au hekaya, lakini kama hatua za mwanzo za jadi hii ni za giza na mashaka angeweza kutoa vizazi vingi vya uungwana (usharifu) safi na halisi; alichipukia kutoka kwenye kabila ya Quraish na ukoo wa Hashim ulio maarufu sana wa Waarabu, mabwana wa Makka, wasimamizi warithi wa Al-Kaaba.
(The Decline and Fall of the Roman Empire)
Hashim alikuwa na ndugu yake mdogo alikuwa akiitwa Al-Muttalib, mtoto wa Abd Manafi. Kwa kipindi, alikuwa ndiye mkuu wa ukoo huo, na alipofariki mpawe - Abdul Muttalib - mtoto wa Hashim, alimfuatia yeye kama mkuu mpya wa ukoo huo. Abdul Muttalib alidhihirisha sifa zote zilizoyafanya majina ya baba na babu yake kuwa makubwa na maarufu.
Kama ilivyoonekana kabla, mji wa Makka kama Arabia yote, ulikuwa hauna serikali wala mtawala, lakini ulimilikiwa na kabila la Quraish. Quraish ilitokana na koo kumi na mbili, na Banu Hashim ulikuwa mmoja wao. Kwa kupinga uharibifu wa tabia wa nyakati; watu wa ukoo wa Banu Hashim, walikumbuka, nusu karne kabla ya kuzaliwa Muhammad, kufanya juhudi za kujaribu kuzuia kuanguka kwa maadili ya Waarabu na kuimarisha hali ya kijamii, kiuchumi na ukuzi wa akili ya nchi hiyo. Wao, kwa hiyo, walibuni au kuunda shirikisho la wenye maadili. Malengo makuu ya shirikisho yalikuwa kuzuia vita kutokana na kugawanyika na kuwalinda wanyonge na wasio na ulinzi kutoka kwa maadui.
Hawa Banu Hashim vilevile walijishughulisha katika ustawi wa uchumi wa Waarabu na walianzisha mfumo wa biashara na nchi majirani kwa kutuma misafara kwenda Syria wakati wa kiangazi na Yemen wakati wa kipupwe, kama ilivyoelezwa kabla. Misafara iliondoka Makka ikiwa imebebeshwa bidhaa kama matunda ya tende, lijamu na hatamu za farasi na ngamia, mablanketi yaliyotengenezwa kwa sufi au manyoya ya ngamia; manukato na mimea yenye kunukia uzuri, viungo, ubani, pembe na ngozi za wanyama wa jangwani, na farasi wa ukoo safu. Walirudi na nguo, mafuta ya zeituni, silaha, kahawa, matunda na nafaka.
Yote haya, shirikisho la wenye maadili na biashara ya misafara yalikuwa, bila ya ubishi, ni zawadi kubwa ya Bani Hashim kwa Waarabu. Lakini zawadi kubwa mno sio tu kwa Waarabu, bali kwa dunia nzima, ilikuwa iwe ni yule mtoto aliyekuwa aitwe Muhammad mwana wa Abdullah ibn Abdul Muttalib na Amina binti Wahab, alikuwa aje kuwa mfadhili mkuu, sio tu kwa Waarabu bali kwa wanadamu wote. Moja ya matukio maarufu lilitokea wakati wa wajibu wa Abdul Muttalib kama msimamizi wa Al-Kaaba, lilikuwa ni uvamizi wa Makka toka kwa jeshi la Kihabeshi likiongozwa na yule jemadari wa Kikristo, Abraha. Hilo jaribio la kuiteka Makka lilishindwa kama ilivyoelezwa katika Aya ya Qur'an Tukufu ifuatayo:
"...Na akawapelekea juu yao, ndege makundi makundi, wakawatupia mawe ya udongo mkavu. Na akawafanya kama majani yaliyotafunwa tafunwa." (Sura ya 105: 3-5 )
Kawa vile wavamizi walikuja na tembo (ndovu), ule mwaka wa kampeini yao ulikuja kujulikana kama "Mwaka wa Tembo". Huu mwaka wa Tembo uko sawia na mwaka 570 A.D. ambao pia umetokea kuwa ndio mwaka wa kuzaliwa Muhammad, nabii wa wakati ujao. Lile jeshi la uvamizi liliondoka Makka, na masharti ya makubaliano ya kusimamisha vita yakajadiliwa, kwa niaba ya mji wa Makka, na Abdul Muttalib.
Sir John Glubb:
"Mnamo mwaka 570 A.D. Abraha, kaimu mfalme wa Kikristo wa Uhabeshi wa huko Yemen aliingia Makka. Makuraish walikuwa waoga sana au wanyonge mno wa kulipinga jeshi hilo la Kihabeshi na Abdul Muttalib, akiongoza ujumbe, alitoka kwenda kujadiliana na Abraha.

No comments:

Post a Comment